Copa América ni shindalo la aina gani?

Tom Mathinji
3 Min Read

Copa América ni taji la soka ya mataifa ya mabara ya Marekani kusini, kaskazini, kati na visiwa vya Caribbean na linaendeshwa na shirikisho la soka la Marekani ya Kusini CONMEBOL (Confederación Sudamericana de Fútbol).

Hapo awali ni timu 10 pekee za bara la Kusini zilizoshiriki kwa kuwa ndilo asisi wake. Timu hizo ni Argentina, Bolivia, Brazil, Chile, Colombia, Ecuador, Paraguay, Peru, Uruguay na Venezuela huku timu mbili zikialikwa kutoka mabara mengine ili idadi iwe kumi na mbili.

Kwa mujibu wa historia, taji hili lilianzishwa mwaka wa 1916 wakati taifa la Argentina lilikuwa linasherekea karne ya uhuru huku Uruguay ikinyakua taji hilo. Tangu wakati huo, taji hilo limekosa ratiba kamili ya maandalizi yake kama ilivyo kwenye picha.

Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni, iliamuliwa kuwa kipute hicho kitaandaliwa baada ya miaka minne ili kioane na kile cha Uropa na pia kutoingiliana na kile cha kombe la dunia.

Kufanya hivyo pia kutawapa wachezaji fursa ya kupumuzika kama wengine na pia kufuata kalenda ya FIFA. Vile vile, kipute hicho kinashirikisha mataifa sita ya Marekani ya kati, kaskazini na visiwa vya Caribbean yanayoendeshwa na shirikisho la CONCACAF.

Hadi sasa, mabingwa watetezi Argentina na Uruguay wameshinda taji hilo mara 15 kila moja. Brazil wamenyakua mara tisa,Chile, Paraguay na Peru mara mbili kila moja kisha Bolivia na Colombia mara moja kila Moja.

Zaidi ya hayo, nyota wa Uruguay wanaongoza kwa kunyakua taji hiyo kama vile Angel Romano(6), Pascual Somma (4), Alfredo Zibechi (4), Hector Scarone (4) na Jose Nasazzi (4). Gwiji wa Agertina Guillermo Stabile pia ameshinda mara sita.

Kocha wa zamani wa Argentina Guillermo Stabile ndiye wa pekee kushinda mara sita huku naye kocha Juan Carlos Corazzo akiwa akiandikisha historia ya kushinda taji hilo na mataifa mawili-Uruguay na Argentina namo mwaka wa 1959 wakati shindano hilo liliandaliwa mara mbili nchini Argentina kisha Ecuador.

Katika ufungaji wa magoli; Norbert Martinez wa Argentina (17),Zizinho wa Brazil (17), Lolo Fernandez wa Peru (15), Severino Valera wa Uruguay (15), Pablo Guerrero-Peru (14), Eduardo Vargas -Chile (14),Lionel Messi-Argentina (13), Ademir-Brazil (13), Gabriel Batistuta-Argentina (13),Jair-Brazil (13), Jose Manuel Moreno-Argentina (13) na Hector Scarone-Uruguay (13).

Kwenye maandliIizi, Argentina imeandaa mara tisa, Uruguay na Chile mara saba kila moja.

Mwaka huu, makala ya 48 yameandaliwa nchini Marekani na timu za CONCACAF ni wenyeji Marekani, Canada, Mexico, Costa Rica, Jamaica na Panama.

Ratiba ya awamu za michuano ni kama ifuatavyo;

Juni 14 hadi Julai 14 ni michuano za makundi.
Robo fainali: Julai 3 -6.
Nusu fainali: Julai 9 na 10.
Mechi ya mshindi wa tatu Julai 13.
Fainali: Julai 14.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *