Chuo Kikuu cha Taita Taveta chakuza uelewa wa wachimba madini

Martin Mwanje
1 Min Read
Prof. Maurice Juma Ogada wa Chuo Kikuu cha Taita Taveta

Chuo Kikuu cha Taita Taveta (TTU) kinashirikiana na wafadhili na washikadau wengine kukuza uelewa wa wasanii na wachimba madini wadogo juu ya usalama na uongezaji thamani madini hayo. 

Kutokana na ufadhili wa Idara ya Kitaaluma ya Ujerumani kupitia kwa Kituo cha Ubora wa Uhandisi wa Uchimbaji Madini na Usimamizi wa Rasilimali (CEMERM), chuo hicho kimeshirikiana na vyuo vikuu viwili vya Ujerumani kukuza ujuzi na uelewa wa wachimba madini.

Maurice Juma Ogada ni Profesa wa Kilimo na Uchumi wa Rasilimali katika Chuo Kikuu cha TTU.

Akizungumza mjini Kakamega wakati wa kongamano la siku tatu la utoaji mafunzo ya kiufundi kwa wasanii na wachimba madini wadogo wadogo,  Prof. Ogada alisema kutokana na ukosefu wa udhibiti wa sekta ya uchimbaji madini, visa vya kutokea kwa ajali za mara kwa mara vimeripotiwa sawia na uharibifu wa mazingira.

Amesema lengo lao ni kuilainisha sekta hiyo kwa manufaa ya nchi.

“Tunataka kuhakikisa wasanii na wachimba madini wadogo wadogo wanafahamu hatari zilizopo kwa mazingira na namna ya kupunguza hatari hizo na kurejesha maeneo ambako uchimbaji madini umekuwa ukiendelea katika hali ya kawaida.”

Share This Article