Chuo cha mafunzo ya matibabu nchini, KMTC kimetangaza kuanza kupokea maombi ya kozi katika mabewa ya chuo hicho kupitia tovuti ya Mamlaka ya Kutoa Nafasi kwa Wanafunzi katika Vyuo Vikuu na Taasisi Zingine za Elimu ya Juu, KUCCPS kuanzia mwezi Septemba mwaka huu.
Wanafunzi waliofanya mtihani wa KCSE kati ya mwaka 2014 na 2023 wanaruhusiwa kutuma maombi yao baina ya Julai 22 na 27 mwaka huu.
Wanaonuia kutuma maombi ambao wanahtaji usaidizi wanahitajika kutembelea mabewa ya KMTC.
Pia wazazi na wanafunzi wanaweza kuzuru afisi za KUCCPS zilizoko jumba la ACK Garden kwenye barabara ya 1st Ngong Avenue Nairobi au kutembelea vituo vya Huduma kote nchini.