Mamlaka ya Anga za Juu nchini (KSA) limethibitisha kuwa chuma cha upana wa mita 2.5 na uzani wa kilo 500 kilichopatikana Makueni jana Jumanne kilitoka kwa roketi.
Chuma hicho cha mviringo kilianguka kutoka angani katika kijiji cha Mukuku, kata ndogo ya Mukuku kata ya Nduluku, eneo la Mbooni katika kaunti ya Makueni.
Tukio hilo lilizua hofu kwa wakazi wa eneo hilo.
Kulingana na KSA, chuma hicho kwa kawaida huanguka baharini au kuchomekea angani baada ya roketi kurushwa angani.