Chol Khan ashinda shindano la ulimbwende Afrika

Marion Bosire
1 Min Read
Joan Okorodudu na Chol Khan

Chol Khan wa asili ya Sudan Kusini mkazi wa kambi ya wakimbizi ya Dadaab ndiye mshindi wa shindano na ulimbwende Afrika almaarufu “Africa’s Next Super Model”.

Fainali za mashindano hayo ziliandaliwa kwenye hoteli ya Radisson Blue jijini Nairobi Jumamosi Oktoba 28, 2023.

Mrembo huyo wa umri wa miaka 19, alitunukiwa zawadi kuu ya pesa ambayo ni shilingi 752000 alipowapiku wenzake 36 kwenye mashindano hayo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na watu tajika kutoka ubalozi wa Sudan Kusini humu nchini pamoja na vongozi kama vile mbunge wa Dagoretti Kaskazini Beatrice Elachi na afisa mkuu mtendaji wa shirika la hakimiliki za muziki nchini Ezekiel Mutua kati ya wengine wengi.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wakimbizi UNHCR nalo liliwakilishwa kwenye hafla hiyo.

Binti huyo sasa anajiunga na wanamitindo na walimbwende wa Sudan Kusini kama vile Grace Bol, Ajak Deng, Anok Yai ambao wamebobea kwenye sekta ya uonyeshaji mavazi na bidhaa ulimwenguni.

Share This Article