Mwanamuziki wa Uganda Dax Vibez ametangaza eneo jipya la maandalizi ya tamasha lake baada ya utata uliozingira eneo la awali.
Mwanamuziki huyo alitumia mitandao ya kijamii kutangaza kwamba tamasha hilo la Agosti 29, 2025 litaandaliwa katiwa uwanja wa maonyesho wa UMA huko Lugogo.
“Tarehe ile ile, eneo bora, nguvu zaidi,” aliandika mwanamuziki huyo kwenye Facebook.
Awali tamasha hilo lilikuwa limepangiwa kuandaliwa katika hoteli ya Africana, lakini wasimamizi wa hoteli hiyo wakalifutilia mbali.
Dax alikuwa amesema kwamna hakufahamu sababu za kufutiliwa mbali kwa tamasha hilo lakini baadaye ilibainika kwamba wamiliki wa hoteli hiyo ndio waliamua kutompa fursa hiyo.
Juni 28, 2025 Dax alichapisha ujumbe kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii kulalamikia kufutiliwa mbali kwa tamasha lake ambapo aliandika, “Baada ya miezi tisa ya matangazo na uwekezaji, Hotel Africana imetupilia mbali tamasha langu. Sijui cha kufanya”.
Hoteli hiyo ya Africana imefahamika sasa kwa hatua za kufutilia mbali matamasha la Dax likiwa la pili baada ya lile la Alien Skin mwezi Februari mwaka huu.