Kiungo mshambulizi wa timu ya taifa ya Kenya kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 Aldrine Kipchirchir Kibe,t amesaini mkataba wa miaka minne na timu akiba ya Celta Vigo ya Uhispania hadi mwaka 2029.
Kibet aliye na umri wa miaka 18, alisaini mkataba huo jana baada ya kupasi majaribio.
Kabla ya kujiunga na Celta, Kibet alikuwa katika Akademia ya Nastic nchini Uhispania, alikojiunga punde baada ya kuiongoza shule ya St Anthony Boys Kitale mwaka 2023, kutwaa ubingwa wa kitaifa katika mashindano baina ya shule za sekondari nchini.
Aidha, alitawazwa mchezaji bora mwaka huo wa 2023 na pia mfungaji bora kwa magoli matano.
Kibet ,ataanzia katika timu ya akiba ya Celta Vigo inayoshiriki Ligi Kuu Uhispania, kabla ya kujumuishwa kwenye kikosi cha kwanza.
 
					 
			 
                                
                              
		 
		 
		 
		