China yaadhimisha miaka 80 ya ushindi dhidi ya uvamizi wa Japani kwa gwaride kubwa la kijeshi

KBC Digital
2 Min Read

Leo Septemba 3, saa tatu asubuhi, shughuli kubwa za kuadhimisha miaka 80 ya ushindi wa vita ya watu wa China dhidi ya uvamizi ya Japani na ushindi wa vita ya dunia dhidi ya ufashisti, ikiwa ni pamoja na gwaride kubwa la kijeshi, zimefanyika katika Uwanja wa Tian’anmen mjini Beijing, China.

Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ambaye pia ni Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamisheni Kuu ya Kijeshi ya Kamati Kuu ya Chama, Xi Jinping, ametoa hotuba muhimu na kukagua gwaride hilo lililoshirikisha vikosi mbalimbali vya jeshi.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Kukumbuka Historia, Kutoa Heshima kwa Mashujaa Waliojitoa Mhanga, Kuthamini Amani na Kufungua Siku za Mbele”.

Wakuu wa nchi na viongozi wa serikali 26 wamehudhuria maadhimisho hayo. Maspika wa bunge, manaibu waziri wakuu, na wawakilishi wa ngazi ya juu kutoka baadhi ya nchi, wasimamizi wa mashirika ya kimataifa na viongozi wastaafu wa nchi na serikali wamealikwa kuhudhuria shughuli hizo.

Mbali na hawa, mabalozi na waambata wa kijeshi wa nchi mbalimbali nchini China, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa nchini China, pamoja na marafiki wa China au wawakilishi wa jamaa za wale waliofariki kutoka nchi 14 zikiwemo Russia, Marekani, Uingereza, Ufaransa na Canada wamealikwa kuhudhuria shughuli hizo.

Miaka 80 iliyopita, baada ya miaka 14 ya mapambano magumu na ya kumwaga damu, taifa la China lilipata ushindi mkubwa katika vita dhidi ya uvamizi wa Japan, ikiashiria ushindi kamili katika vita ya dunia dhidi ya ufashisti. Vita dhidi ya uvamizi wa Japan ilianza mapema zaidi na kudumu kwa muda mrefu zaidi, ikiifanya China kuwa medani kuu ya vita ya dunia dhidi ya ufashisti katika Mashariki mwa Dunia, na kutoa mchango wa kihistoria kwa ushindi wa vita ya dunia dhidi ya ufashisti.

KBC Digital
+ posts
Share This Article