Cheptegei agura mbio za uwanjani baada ya kutwaa dhahabu ya tatu ya dunia ya mita 10,000

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mara tatu wa dunia katika mbio za mita 10,000 Joshua Cheptegei wa Uganda, ametangaza kuhama mashindano ya uwanjani baada ya kutwaa dhahabu ya tatu ya dunia kwa mpigo Jumapili usiku mjini Budapest Hungary.

Cheptegei aliye  na umri wa miaka 26 alistahimili ukinzani mkali na kuhifadhi taji ya dunia mjini Budapest Jumapili, licha ya kutokuwa katika ubora wake msimu huu.

Mwanariadha huyo ambaye ni Inspekta jenerali wa kikosi cha polisi nchini Uganda ni mwanariadha wa nne kushinda mataji matatu mtawalia ya dunia katika mbio hizo za mizunguko 24 baada ya Wahabeshi  Haile Gebrselassie na Kenenisa Bekele,walioshinda mataji manne ya dunia kila mmoja na Mwingereza Mo Faraha.

Katika mashindano ya uwanjani Cheptegei ameshinda dhahabu 3 na fedha moja ya dunia katika mita 10,000 dhahabu moja  na fedha moja ya Olimpiki katika mita 5,000 na 10,000 mtawalia na dhahabu 2 za michezo ya jumuiya ya madola katika mbio za mita 5,000 na mita 10,000.

Cheptegei sasa atahamia mbio za barabarani na zile za marathon .

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *