Wakenya Ruth Chepngetich na Benson Kipruto watarejea katika barabara za Chicago nchini Marekani Jumapili jioni majira ya Afrika Mashariki kutetea mataji ya mbio hizo waliyotwaa mwaka 2022.
Chepngetich anayewinda taji ya tatu mtawalia ya Chicago Marathon atamenyana na bingwa wa London Marathon mwaka huu Sifan Hassan kutoka Uholanzi, Genzebe Dibaba kutoka Ethiopia na wenzake Tadu Teshome na Ababel Yeshaneh.
Upande wa wanaume, Kipruto atalenga kuwasawazisha rekodi ya marehemu Samuel Wanjiru ya mwaka 2010 kwa kushinda mbio hizo.
Kipruto atakabiliana na Wakenya wenza Kelvin Kiptum, John Korir, Wesley Kiptoo na Wahabeshi Seifu Tura na Kinde Atanew.