Cynthia Chepngeno ndiye mshindi wa mbio za mita 5,000 katika siku ya kwanza ya mkondo wa nne wa mashindano ya chama cha riadha Kenya na Betika uwanjani Afraha, Nakuru.
Chepngeno wa kutoka jeshi ameziparakasa mbio hizo kwa dakika 15 sekunde 28.6, akifuatwa na Gladys Jeptepkeny wa Kenya Navy, kwa dakika 15 sekunde 29.6, nukta 3 mbele ya Cynthia Chepkurui wa kambi ya Lemotit aliyeridhia nafasi ya tatu.
Mercy Chepkemoi na Rebecca Mwangi walimaliza katika nafasi za nne na tano mtawalia.
Mkondo huo wa nne ambao ni wa mwisho kuandaliwa mashinani utakamilika kesho .