Chelugui: Serikali italainisha sekta ya kahawa

Tom Mathinji
1 Min Read

Waziri wa ustawi wa vyama vya ushirika, biashara ndogo na za kadri Simon Chelugui, ameahidi kutekeleza marekebisho muafaka ya kulainisha sekta ya kahawa nchini.

Kulingana na Waziri huyo baadhi ya marekebisho hayo,  ni pamoja na uzinduzi wa hazina ya sekta hiyo, wakfu wa utafiti wa kahawa pamoja na bodi ya kahawa nchini na uzinduzi wa vyama 14 vya ushirika vya wakulima wa zao hilo.

Akiongea katika eneo la Kangundo kaunti ya Machakos wakati wa uzinduzi wa hazina hiyo, Chelugui alisema wakfu huo wa utafiti utawezesha wakulima kuchagua aina ya mbegu ya kahawa inayoweza kukua vyema katika maeneo yao.

” Tutatimiza ahadi yetu ya kuimarisha sekta ya kahawa kwa manufaa ya wakulima na uchumi wa taifa kwa jumla,” alisema Waziri Chelugui.

Alisema hatua hiyo itatekelezwa kupitia vyama vyao vya ushirika na mswada wa kahawa ambao tayari umewasilishwa bungeni.

Waziri pia aliwaonya wafanyibiashara ambao wamekuwa wakiwalagai wakulima wa kahawa akisema watakabiliwa vilivyio kupitia sheria mpya zitakazozinduliwa katika sekta ya hiyo

Share This Article