Mabingwa wa Kombe la Dunia,Chelsea wamemteua Xabi Alonso, kuwa meneja kwa kandarasi ya miaka minne kuanzia Julai mosi mwaka huu.
Alonso hajakuwa na kazi tangu afurushwe kutoka Real Madrid, Januari 12 mwaka huu, kufuatia msururu wa matokeo mabaya.
Awali kocha huyo aliye na umri wa miaka 44, alikuwa ameshinda taji ya ligi Kuu Ujerumani akiwa na Bayer Leverkusen, kabla ya kuhamia Madrid.
Chelsea imehiari kumteua Alonso, baada ya kuwa na msimu mbovu huku wakikosa kufuzu kwa ligi ya Mabingwa msimu ujao .
Aidha, The Blues huenda pia wakose kufuzu kwa Europa League, wakishikilia nafasi ya 9 kwa alama 49.
Wakati uo huo Manchester United, imemteua meneja wa muda Michael Carrick, baada ya kufanya vyema na klabu hiyo akiwa kaimu.
Carrick anatarajiwa kusaini mkataba wa aidha miaka miwili au miaka mitatu.