Arteta asikitikia hatua ya Arsenal kutosajili wachezaji wapya

Martin Mwanje and Radio Taifa
1 Min Read
Mikel Arteta - Kocha wa Arsenal

Kocha wa timu ya Arsenal Mikel Arteta amesikitikia hatua ya klabu yake ya kutowasajili wachezaji wapya wakati wa kipindi kilichopita cha usajili.

Hata hivyo, amesifu nidhamu ya wachezaji wake.

Arsenal imekuwa ikikabiliwa na shinikizo la kuwasajili washambulizi kutokana na timu hiyo kukosa makali katika safu yake ya mbele.

Hii ni hasa baada ya wachezaji wake nyota Gabriel Jesus kujeruhiwa mwezi uliopita huku Bukayo Saka akiwa bado anauguza jeraha pajani.

Arteta alisema safu ya ushambulizi ya timu yake italazimika kutia bidii na kwamba anaweza kujaribu mbinu tofauti kwa sababu ya majeraha.

Wachezaji watatu waliondoka Arsenal wakati wa kipindi cha usajili wa wachezaji huku mabeki Ayden Heaven na Josh Robinson wakijiunga na Manchester United na Wigan Athletic mtawalia.

Mshambulizi Marquinhos wa Brazil alijiunga na klabu ya Cruzeiro kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu.

Arsenal inashikilia nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya soka nchini Uingereza kufuatia ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Manchester City Jumapili iliyopita, ikiwa alama sita nyuma ya vinara Liverpool.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article