Chebet na Wanyonyi watwaa ubingwa Xiamen Diamond League

Dismas Otuke
2 Min Read

Mshindi wa nishani ya Fedha ya Dunia katika mita 800 Emmanuel Wanyonyi na mshindi wa medali ya shaba katika mita 5,000 Beatrice Chebet wameibuka washindi katika mkondo wa 12 wa mashindan ya Xiamen Diamond League nchini Uchina Jumamosi adhuhuri.

Wanyonyi ameziparakasa mbio hizo kwa muda wa dakika 1 sekunde 43 nukta 20 ikiwa rekodi mpya na pia muda wa kasi ulimwenguni, akimpiku bingwa wa dunia Marco Arop wa Canada aliyemaliza wa pili kwa dakika 1 sekunde 43 nukta 24, huku Robert Benjamin wa Ufaransa akiambulia nafasi ya tatu.

Emmanuel WANYONYI, Marco AROP

Chebet ambaye pia ni bingwa wa jumuiya ya madola ameshinda mbio za mita 3,000 akiweka rekodi mpya,muda bora ulimwenguni na muda bora wa kibinafsi wa dakika 8 sekunde 24 nukta 03, akifuatwa na Laura Galvan wa Mexico huku Margaret Akidor wa Kenya akichukua nafasi ya tatu.

Amos Serem na mshindi wa nishani ya shaba ya dunia  Abraham Kibiwott wamemaliza katika nafasi za tau na nne kwenye fainali ya mita 3,000 kuruka viunzi na maji .

Bingwa wa dunia Soufiane El Bakkali wa Morocco amenyakua ushindi.

Nelly Jepchirchir amemaliza wa pili katika mita 1500 wanawake akirekodi muda wa dakika  3 sekunde 57 nukta 72 ,nyuma ya mshindi Frewyeni Hailu wa Ethiopia aliyetumia dakika 3 sekunde 56 nukta 56 .

Website |  + posts
Share This Article