Chebet avunja rekodi ya dunia ya kilomita 5

Dismas Otuke
0 Min Read

Bingwa wa dunia wa mbio za Nyika Beatrice Chebet, alifunga mwaka 2023 kwa matao ya juu baada ya kuvunja rekodi ya dunia ya kilomita 5 katika shindano la Cursa dels Nassos, mjini Barcelona Uhispania Jumapili.

Chebet aliye na umri wa miaka 23 amesajili rekodi mpya ya dunia ya dakika 14 na sekunde 13, akivunja rekodi ya Mwethiopia Senebere Teferi ya dakika 14 na sekunde 29.

Share This Article