Bingwa wa dunia wa mbio za nyika Beatrice Chebet, ametwaa dhahabu ya kilomita 5 katika makala ya kwanza ya mashindano ya dunia ya mbio za barabarani, akiweka rekodi mpya ya dakika 14 na sekunde 35 .
Mashindano hayo yameandaliwa Jumapili mjini Riga nchini Latvia huku Chebet ambaye pia ni mshindi wa nishani ya fedha ya dunia katika mita 5,000 mwaka huu, akitwaa uongozi katika kilomita ya 4 na kukata utepe wa kwanza.
Lillian Kasait Rengeruk wa Kenya ameshinda medali ya fedha kwa muda wa dakika 14 na sekunde 39, huku Elgayehu Taye wa Ethiopia aliyekuwa akiongoza kutoka mwanzo akiridhia nsihani ya shaba.