Chebet atawazwa mwanaspoti bora wa Agosti

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mara mbili wa Olimpiki Beatrice Chebet ndiye mwanaspoti bora wa mwezi Agosti wa tuzo ya chama cha wanahabari wa michezo LG/SJAK, baada ya kusajili matokeo bora katika michezo ya Olimpiki ya Paris,Ufaransa.

Chebet aliandikisha historia kuwa Mkenya wa kwanza kushinda dhahabu ya mita 5,000 na miat 10,000 katika makala moja ya Olimpiki na pia mshindi wa pili wa dhahabu ya Olimpiki ya mita 5,000 baada ya Vivian Cheruiyot mwaka 2016 nchini Brazil.

Bingwa huyo mara mbili wa Dunia katika mbio za nyika aliwashinda mabingwa wa Olimpiki Faith Kipyegon na Emmanuel Wanyonyi miongoni mwa wanamichezo wengine , ili kushinda tuzo ya tano ya LG/SJAK.

Chebet amerejea nchini mapema leo baada ya kukamilisha msimu wake wa mashindano ya uwanjani alipotwaa ubingwa wa tuzo ya Diamond mjini Brussels ,Ubelgiji Jumamosi iliyopita.

Share This Article