Chebet alenga dhahabu ya dunia mwaka ujao mjini Tokyo

Mwanariadha huyo aliye na umri wa miaka 24 pia anajivunia kushinda dhahabu tatu za dunia katika mbio za nyika moja akiwa chipukizi na mbili za kibinafsi katika kilomita 10.

Dismas Otuke
2 Min Read

Bingwa wa dhahabu mbili za Olimpiki Beatrice Chebet amesema anawinda dhahabu telezi kwenye mashindano ya Dunia ya mwaka ujao mjini Tokyo Japan.

Chebet ambaye aliyenyakau dhahabu katika mita 5,000 na 10,000 katika michezo ya Olimpiki mwaka huu mjini Paris Ufaransa, amesema bado hajaafikia upeo wake.

Aidha Chebet ametaja mwaka 2024 kuwa msimu wa kufana na kudokeza uwezekano wa kuvunja rekodi ya dunia katika mita 5,000 au 10,000 endapo atapata fursa mwafaka mwaka ujao.

“2024 Imekuwa season yenye baraka sana kwangu kuleta gold mbili za Olympics,Ihope 2025 itakuwa nzuri pia kwangu”,amesema Chebet

Chebet ameongeza kuwa”Bado sijafika kwenye nina enda ,after kukimbia World Championship mwaka 2022 nikapata Silver ilinipa motisha na sasa after kuvunja rekodi ya Dunia na kushinda dhahabu za olimpiki nafurahia sana,target yangu probably nipate hiyo gold ya World Championship next year”.

Mwanariadha huyo aliye na umri wa miaka 24 pia anajivunia kushinda dhahabu tatu za dunia katika mbio za nyika moja akiwa chipukizi na mbili za kibinafsi katika kilomita 10.

Chebet ambaye ni afisa wa polisi wa Utawala pia alinyakua medali ya fedha ya Dunia katika mita 5,000 mwaka 2022 ,kabla ya kushinda shaba mwaka jana mjini Budapest.

Kando na kunyakua dhahabu mbili za Olimpiki mwaka huu ,Chebet pia alishinda tuzo ya Diamond katika mita 5,000 na kuweka rekodi mpya ya dunia ya dakika 28 sekunde 54.14 mjini Eugene Marekani katika mwaka 2024.

Pia tayari Chebet amefungua msimu wake wa mwaka 2024-2025 kwa uhsindi alipotwaa ubingwa katika mbio za Cross International De Italica wiki jana mjini Seville Uhispania ,akinyakua taji ya tatu kwa mpigo kwenye mbio hizo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *