Charles Keter ateuliwa kuwa mshauri wa Rais

Tom Mathinji
1 Min Read
Charles Keter.

Aliyekuwa waziri Charles Keter  amemshukuru Rais William Ruto kwa kumteua kuwa mshauri wake wa maswala ya maziwa makuu.

Keter ambaye aliwania wadhifa wa ugavana wa kaunti ya Kericho bila mafanikio, alisema uteuzi huo wake ni ishara ya kwamba Rais Ruto ana imani naye.

“Kwa unyenyekevu namshukuru Rais William Ruto kwa kuniyeua kuwa mshauri wake wa maswala ya maziwa makuu,”alisema Keter.

Rais Ruto alimteua Keter ambaye alikuwa waziri wa kawi na pia ugatuzi katika serikali iliyopita, kuwa mshauri wake wa maswala ya maeneo ya maziwa makuu.

Keter alikuwa waziri wa kwanza kujiuzulu ili kuwania ugavana wa kericho, lakini alipigwa kumbo na Dkt. Erick Mutai.

Keter alichaguliwa waziri wa kawi katika serikali iliyopita, kabla ya kupelekwa kwa wizara ya ugatuzi katika mabadiliko yaliyofanywa mwezi Februari mwaka 2022.

TAGGED:
Share This Article