Chapa Dimba yatua Kaskazini Mashariki

Tom Mathinji
2 Min Read
Chapa Dimba yatua kaskazini Mashariki.

Fainali ya Chapa Dimba kanda ya Kaskazini Mashariki imeanza kwa msururu wa mipango inayolenga kubadilisha maisha ya jamii katika eneo hilo.

Mipango hiyo inahusisha kambi za matibabu ya bure ambazo zilifanyika siku ya Jumamosi katika hospitali ya Garissa Level 5. Pia kutakuwa na warsha ya mafunzo kuhusu fedha itakayofanyika eneo la Hola.

Fainali hizo za kandanda, zitafanyika Februari 24 na 25 katika Chuo Kikuu cha Garissa, kaunti ya Garissa.

“Ni jambo la kufurahisha kuona jinsi mchezo wa soka umeendelea kuimarik katika ukanda huu. Katika historia ya Chapa Dimba, hii ni mara ya kwanza tunashuhudia, zaidi ya timu 280 kutoka Kaskazini Mashariki zikisajiliwa kushiriki michuano hiyo. Michuano hiyo haitumiki tu kukuza vipaji bali pia kubadilisha maisha ya jamii nzima. Ndio maana leo, tunaanza rasmi na msururu wa shughuli za kushirikisha jamii, zikiwemo kambi za matibabu bila malipo, pamoja na programu za elimu ya kidijitali na kifedha zinazolenga kuwawezesha wateja wetu katika eneo hili,” alisema Peter Ndegwa, Afisa Mkuu Mtendaji wa Safaricom PLC.

Wachezaji na makocha watapokea mafunzo kuhusu ukuzaji wa ujuzi, maadali ya kijamii, ushirikiano na uongozi.

Wakufunzi watapata ujuzi wa kimafunzo, mbinu za michezo na jinisi ya kuzungumza na wachezaji.

Wiki iliyopita, watu 3,300 walipokea matibabu katika kambi ya matibabu kaunti ya Garissa, yaliyojumuisha  uchunguzi wa shinikizo la damu, saratani, na hali jumla ya afya  mwilini.

TAGGED:
Share This Article