Harambee Stars ya Kenya itawaandaa Barea kutoka Madagascar leo katika robo fainali ya kwanza ya makala ya nane ya kipute cha CHAN kuanzia saa kumi na moja jioni.
Kenya inakutakana na Madgascar kwa mara ya pili katika historia wakijuvunia kuwashinda Barea goli moja bila jibu katika mechi ya kirafiki mwaka 2019.
Harambee Stars iliongoza kundi A kwa pointi 10 wakishinda mechi tatu na kusajili sare moja .
Upande wake Madagascar ilimaliza ya pili katika kundi B kwa alama 7 ikishinda mechi 2 kutoka sare moja na kupoteza moja.

Robo fainali ya pili itakuwa kati ya mabingwa mara mbili Morocco, dhidi ya Taifa Stars ya Tanzania uwanjani Benjamin Mkapa kuanzia saa ,mbili usiku.
Morocco walimaliza nafasi ya pili kundini A kwa pointi 9 huku Tanzania wakiongoza kundi B kwa alama 10.