Celine Dion: Nitarejea katika muziki, niko tayari

Tom Mathinji
1 Min Read
Celine Dion atangaza kurejea kwenye muziki.

Mwanamuziki tajika Céline Dion ametangaza kurejea kwenye muziki, baada kugunduliwa kuugua ugonjwa usiotibika miaka minne iliyopita.

Dion aliyesifika kwa nyimbo kama vile Because You Loved Me, miongoni mwa nyingine, atapanda jukwaani mwezi Septemba na Octoba mwaka huu  katika ukumbi wa Paris La Défense Arena nchini Ufaransa.

Katika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram, Dion alitaja kurudi kwake kwenye muziki  kama zawadi bora zaidi ya maisha yake.

“Niko tayari kufanya hivi, ninahisi vyema, nina nguvu na ninafuraha licha ya kwamba ninahisi wazsiwasi kidogo,” alisema mwanamuziki huyo.

Dion, hajaimba kwenye tamasha lolote tangu kushiriki kwenye hafla iliyoandaliwa New Jersey mnamo Machi 8, 2020.

Awali,Dion ambaye ni raia wa Canada, alitangaza kuambukizwa ugonjwa wa Stiff Person Syndrome (SPS) mwezi Disemba mkwaka 2022.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, alisema hali hiyo iliathiri  kila sehemu ya maisha yake.

TAGGED:
Share This Article