CECAFA: Makinda wa Kenya waizaba Sudan

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji Kenya wameanza mashindano ya kuwania kombe la CECAFA kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 18 kwa ushindi wa Mabao matano kwa bila dhidi ya Sudan, katika mchuano wa kundi A uliosakatwa Jumamosi Alasiri katika uwanja wa Mamboleo, kaunti ya Kisumu.

Louise Ingavi alifungua karamu ya magoli kwa Kenya kwa bao la dakika ya saba kabla ya Tyrone Kariuki kuongeza la pili dakika ya 29.

Aldrine Kibet alipachika la tatu dakika ya 33 kisha Ingavi akabusu nyavu kwa mara ya pili muda mfupi kabla ya mapumziko.

Wachezaji wa Kenya washerehekea bao

Elly Owande alikamilisha ushindi maridhawa kwa Kenya dakika ya 88 kwa bao la tano.

Kenya watarejea uwanjani Jumanne ijayo dhidi ya Rwanda kabla ya kuhitimisha ratiba Disemba mosi dhidi ya Somalia.

Share This Article