Shirikisho la soka barani Afrika limetangaza zawadi ya donge nono kwa timu zitakazoshiriki makala ya kwanza ya kipute cha ligi ya soka Afrika (AFL), kitakachoandaliwa kuanzia Oktoba 20 mwaka huu.
Mabingwa watatunukiwa dola milioni 4 za Marekani nafasi ya pili dola milioni 3, na dola 1 nukta 7 kwa timu zitakazofika nusu fainali na dola milioni 1 kwa timu timu zitakashindwa katika robo fainali.
Simba Sports Club ya Tanzania itawaalika mabingwa wa Afrika Al Ahly kutoka Misri, katika duru ya kwanza ya robo fainali katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Katika michuano mingine ya robo fainali Toupiza Mazembe ya Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo itamenyana na Esperance ya Tunisaia,Wydad Athletic Club ya Moroco ikabane koo na Enyimba ya Nigeria huku Petro Atletico ya Angola ikipambana na Mamelodi Sundowns kutoka Afrika Kusini.