CAF yaiadhibu Libya huku Nigeria wakipewa alama za ubwete

Dismas Otuke
1 Min Read

Bodi ya nidhamu ya Shirikisho la soka barani Afrika CAF imeiadhibu Libya vikali kutokana na mechi ya kufuzu kwa AFCON mwaka 2025 dhidi ya Nigeria.

Shirikisho la kandanda nchini Libya limetozwa faini ya dola 50,000 inayopaswa kulipwa ndani ya siku 60.

Nigeria pia wamepewa ushindi wa ubwete wa mabao 3-0, dhidi dhidi ya Libya .

Mechi hiyo nambari 87 iliratibiwa kusakatwa Oktoba 15 Mjini Benghazi, lakini wenyeji wakashindwa kutoa mpangilio wa kiusalama na mapokezi kwa wageni Nigeria.

Share This Article