CA: Rununu zinazotumiwa na kuingizwa nchini sharti ziwe za Type C

Dismas Otuke
1 Min Read

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (CA) imesema kuwa ni sharti kwa simu zote za rununu zinazouzwa nchini ziwe za aina ya Type C.

Aidha, CA imeweka bayana kuwa watengezaji wa simu zinazouzwa humu nchini lazima wafuate agizo hilo ili kuwahakikishia wateja usalama wao na kuwa na simu zenye mitandao yenye nguvu.

Mkurugenzi Mkuu wa CA David Mugonyi, ameongeza kuwa simu za rununu na vifaa vinavyoambatana nazo havifai kutengenezwa kwa madini ya lead, mercury, cadmium au madini yoyote hatari kwa usalama wa watumiaji.

TAGGED:
Share This Article