Msanii maarufu wa asili ya Nigeria Damini Ebunoluwa Ogulu maarufu kama Burna Boy amesema kwamba yeye sio msanii wa Nigeria tu.
Dhana hiyo kulingana naye ni ya kumkosea heshima.
Mshindi huyo wa tuzo ya Grammy anasema kila anaporejelewa kama msanii wa Nigeria anahisi kwamba ndoto zake hazijatimia.
Anasema yeye ni msanii wa Afrika na ndoto yake ni kuhakikisha Afrika inaungana.
“Ninapoona watu wa Nigeria na Afrika Kusini wakipigana kila mara chozi hunitoka. Amerika imeafikia ufanisi leo kwa sababu majimbo yote yameungana na hakuna tofauti.” alisema Burna Boy.
Aliongeza kusema kwamba uthabiri wa Marekani unatokana na umoja wao na kila mtu anaposema anatoka Marekani huwa haulizwi jimbo lake.
Mwanamuziki huyo alisema kwamba siku ambayo bara Afrika litakuwa “United States of Africa” basi litakuwa nchi thabiti saidi ulimwengini.
“Muziki wetu utakua na utapendeka ulimwenguni kote.” alimalizia mwimbaji huyo akisema Waafrika ni watu wenye nguvu lakini kinachowadhoofisha ni ukosefu wa umoja.