Bunge laanza kuwapiga msasa Makatibu wa Wizara

Dismas Otuke
1 Min Read

Kamati za bunge zimeanza shughuli ya kuwasaili Makatibu wateule mapema leo, ambapo maafisa 11 watahojiwa .

Makatibu watakaosailiwa leo ni pamoja na Aden Abdi wa usafiri wa majini, Stephen Isaboke wa utangazaji na mawasiliano, Michael Lenasalon wa ugatuzi, Dkt. Ouma Oluga wa huduma za matibabu na Ahemd Ibrahim wa uratibu wa huduma za serikali ya kitaifa .

Wengine watakaopigwa msasa ni Professa Abdulrazak Shaukat wa idara ya Sayansi, Utafiti na Uvumbuzi, Jane Imbunya wa Utumishi wa Umma na Nguvukazi, Jacobs Fikirini wa masuala ya vijana, Regina Ombam wa biashara, Cyrell Wagunda wa uwekezaji na usimamizi wa raslimali za umma na Boniface Makokha wa Uchumi na mipango.

Makatibu hao wataapishwa kuanza kutekeleza majukumu yao punde baada ya kuidhinishwa na bunge.

 

Website |  + posts
Share This Article