Bunge la Ulaya (EU) kesho, Mei 7, linatarajia kujadili kwa dharura kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, na hatari ya hukumu yake iwapo atapatikana na hatia ya uhaini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Bunge hilo, mjadala huo utafanyika kesho kati ya saa saba mchana hadi saa nne usiku .
Baada ya mjadala huo, Wabunge wa Ulaya wataandaa na kupiga kura kuhusu mjadala huo wa kesi ya Lissu.