Bunge la kaunti ya Busia limeidhinisha kwa kauli moja, walioteuliwa kuhudumu katika bodi ya mikopo ya maendeleo ya biashara na katika kamati ya maendeleo ya biashara ya ushirika.
Mwenyekiti wa kamati ya biashara, ushirika na viwanda Boniventure Makokha aliambia bunge kwamba kama kamati walipata kwamba wote walioteuliwa wanatosha kuhudumu huku akiwataka wapitishe hoja yake.
Maoni ya Makokha yalikaririwa na Denzil Musumba mwakilishi wa wadi ya Charcol Kusini, Concepta Omondi aliyeteuliwa,
Isaac Wamalwa wa wadi ya Angurai kaskazini, Gaddy Jakaa wa wadi ya Bukhayo Kaskazini /Walatsi, Monica mung’ala mteule na Jonstone Makabwa wa wadi ya Nangina.
Wawakilishi wadi hao walipongeza kamati ya biashara kwa kuwa wakakamavu kwenye shughuli ya usaili huku wakihimiza haja ya kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kukumbatia vyama vya ushirika.
Walioteuliwa kuhudumu katika bodi ya mikopo ya maendeleo ya biashara ni Gregory Wabwire Akide, Sylvester Okello, Mirriam Wakaya Obura, Lawrence Ekesa Karakacha na Dolofina Amoit.
Wale wa kamati ya maendeleo ya ushirika ni Rachael Atyang Mohmoh, Felix Okhonjo Gabriel, Reuben Ekirapa na Sarah Akumu Muhombe.
Kikao hicho cha bunge kilikuwa chini ya uongozi wa spika Fredrick Odilo ambaye aliagiza kwamba majina ya wateuliwa yawasilishwe kwa mamlaka husika kwa hatua zinazofuata.