Bunge la kaunti ya Busia lazindua mikataba ya kikazi kwa wanachama

KBC Digital
1 Min Read

Bodi ya utumishi ya bunge la kaunti ya Busia, leo imezindua shughuli ya kutia saini kwa mikataba ya utendakazi kwa wafanyakazi wake.

Mwenyekiti wa bodi hiyo ambaye pia ni Spika Fredrick Odilo alitaja umuhimu wa shughuli hiyo akisema itaimarisha utoaji huduma kati ya wafanyakazi hao.

Odilo alisisitiza kwamba hatua hiyo ya kutia saini mikataba ya utendakazi ni hitaji kwa kila mfanyakazi wa serikali akiongeza kwamba imetoka kwa serikali ya kitaifa.

“Tuko hapa leo kuanzisha mpango wa kutia saini mikataba ya utendakazi kwa lengo la kufuatilia utendakazi wa wafanyakazi wote.” alisema Odilo.

Kaimu karani wa bunge hilo Gabriel Erambo ndiye alikuwa wa kwanza kutia saini mkataba wa utendakazi na bodi hiyo akifuatiwa na wakurugenzi na wakurugenzi wasaidizi.

Belinda Makadia mwanachama wa bodi hiyo alihakikishia wafanyakazi kwamba mpango huo sio wakufuatilia yeyote kwa nia mbaya bali ni wa kuimarisha utendakazi.

Wanachama wengine wa bodi waliokuwepo ni Bonface Mamai na Silvanus Alianda. Viongozi katika bunge kama Josephat Wandera kiongozi wa wengi, Zaccheus Kubasu kiongozi wa wachache na Richard Okello pia walikuwepo.

KBC Digital
+ posts
Share This Article