Wabunge watarejelea vikao leo baada ya kusitisha likizo ya muda mrefu,ili kutathmini ripoti ya kamati ya bunge iliyowapiga msasa Mawaziri watatu wapya.
Mawaziri watatu walioteuliwa na Rais William Ruto katika Serikali jumuishi,William Kabogo, Mutahi Kagwe na Lee Kinyajui watabaini hatima yao leo baada kikao hicho cha bunge.
Endapo Mawaziri wateule Kagwe katika Wizara ya kilimo,Kabogo wa Wizara ya Teknolojia ya Habari Mawasiliano na uchumi Dijitali na Kinyanjui wa Biashara wataidhinishwa na bunge, watakuwa huru kula kiapo cha majukumu yao .
Kamati ya bunge la kitaifa pia itawasilisha ripoti ya Mabalozi wateule na uteuzi wa Naibu mwenyekiti wa tume ya huduma za wafanyikazi wa umma.
Wabunge wamekuwa katika likizo ndegu ya miezi miwili kabla ya kuitwa na Spika Moses Wetang’ula.
.