Mabingwa mara tano wa dunia Brazil walisajili ushindi wa mabao 4 kwa moja dhidi ya Guinea, katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyosakatwa katika uwanja wa Espanyol nchini Uhispania.
Brazil walicheza mechi hiyo wakivalia sare nyeusi badala ya zile za kawaida za njano kama njia moja ya kupigana vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, baada ya mshambulizi wao Vinicius kubaguliwa kirangi akiichezea Real Madrid.
Joelinton na Rodrygo walipiga bao moja kila moja katika kipindi cha kwanza naye Serhou Guirassy akakomboa goli moja .
Eder Militao aliongeza bao kipindi cha pili kabl ya Vinicious Junior akaunganisha penati.