Botswana imeteuliwa kuandaa Mbio za Dunia za kupokezana kijiti mwaka ijao kati ya Mei 2 na 3 mjini Gaborone.
Baraza kuu la Shirikisho la Riadha Ulimwenguni limeiteua Botswana leo katika kikao cha 237, kilichoandaliwa mjini Nanjing, China.
Aidha, mji wa Nassau, Bahamas, utaandaa mbio za kupokezana kijiti Duniani mwaka 2028.
Itakuwa mara ya kwanza kwa mashindano hayo ya dunia kuandaliwa barani Afrika.