Boniface Kariuki kuzikwa Ijumaa kaunti ya Murang’a

Tom Mathinji
1 Min Read
Mchuuzi Boniface Mwangi kuzikwa Ijumaa kaunti ya Murang'a.

Boniface Kariuki, mchuuzi wa barakoa aliyepigwa risasi kichwani na polisi wakati wa maandamano Juni 17,2025, atazikwa siku ya Ijumaa, kaunti ya Murang’a.

Mazishi hayo yanajiri siku moja baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), kuidhinisha kesi ya mauaji dhidi ya konstabo wa polisi Klinzy Masinde Barasa kuhusu ya mauaji ya Boniface.

Mshukiwa mwenza Duncan Kiprono, aliachiliwa huru kutokana na ukosefu wa ushahidi.

Kariuki alipigwa risasi kichwani kwa karibu na kupelekwa kwenye Hospitali  ya Kitaia ya Kenyatta alikoanyiwa upasuaji. Alilazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi kwa muda wa wiki mbili kabla ya kuaga dunia.

Uchunguzi wa maiti ulibainisha kuwa Kariuki alifariki kutokana na jeraha kichwani. Vipande vinne vya risasi vilipatikana vimekwama kichwani mwake.

Wakati wa misa ya ukumbusho katika kanisa la Holy Family Basilica, amilia yake ilimtaja kuwa mtu mwenye mtiifu kwa sheria na aliye na bidii.

Website |  + posts
Share This Article