Bongo aruhisiwa kusafiri Ulaya

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Gabon aliyetimuliwa mamlakani Ali Bongo Ondimba, ameachiliwa kutoka kifungu cha nyumbani na kuruhusiwa kusafiri kwenda Ulaya ili kupokea matibabu.

Bongo aliyewekwa chini ya kifungo cha nyumbani tangu Ahosti 30 baada ya serikali yake kupinduliwa siku chache kufuatia kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu, alikuwa amehudumu kwa miaka 14.

Taarifa ya kuachiliwa huru kwa Bongo ilitangazwa na kutiwa saini na Rais mpya wa kijeshi Brice Bongo Oligui, ambaye alikuwa mmoja wa walinzi wake na pia walikuwa wanahusiana kinasaba na Rais huyo wa zamani kutokana na afya yake iliyozorota.

Rais mpya wa kijeshi pia alikuwa mlinzi wa Rais aliyeng’atuliwa mamlakani, marehemu babake Bongo.

Share This Article