Bolsonaro ahukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 27 gerezani kwa kujaribu kubadili matokeo ya Urais

Bolsonaro aliye na umri wa miaka 70 na ambaye amekuwa chini ya kifungo cha nyumbani huenda atumikie kifungo cha miaka 40, baada ya kupatikana na hatia ya makosa manne.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Mstaafu wa Brazil, Jair Bolsonaro amehukumiwa kifungo cha miaka 27 na miezi mitatu gerezani kwa kupatikana na hatia ya kujaribu kubadili matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2022 ili asalie madarakani.

Bolsonaro amepatikana na hatia ya makosa matano ikiwemo kupanga mapinduzi ya kijeshi na kujaribu kumuua Rais Mteulewa wakati huo, Luiz Inácio Lula da Silva.

Majaji wanne kati ya watano wa Mahakama ya Upeo walipiga kura jana ya kuunga mkono kufungwa kwa kiongozi huyo wa zamani wa jeshi huku mmoja pekee akipiga kura ya kumwondolea makosa.

Bolsonaro aliye na umri wa miaka 70 na ambaye amekuwa chini ya kifungo cha nyumbani huenda atumikie kifungo cha miaka 40, baada ya kupatikana na hatia ya makosa manne.

Bolsonaro alikuwa ameapa kuwania Urais mwaka ujao licha ya mahakama ya uchaguzi nchini humo kumpiga marufuku kusimama hadi uchaguzi wa mwaka 2030.

Website |  + posts
Share This Article