Bingwa wa Olimpiki Julien Alfred alakiwa kishujaa nyumbani St Lucia

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa wa Olimpiki katika mbio za mita 100 Julien Alfred amewasili nyumbani kisiwani St Lucia mapema Jumatano na kulakiwa kwa shangwe,mbwembwe, vifijo na nderemo kufuatia matokeo yake bora mwezi jana jijini Paris katika michezo ya Olimpiki.

Alfred alinyakua pia nishani ya fedha katika mita 200 akiwa mwanamichezo wa kwanza kutoka kisiwa hicho kushinda medali ya Olimpiki.

Alfred pia alitawazwa bingwa wa Diamond League msimu huu akimbwaga bingwa wa Dunia Sha Carri Richardson wa Marekani.

Bunge la nchini hiyo mnamo Septemba 16 liliidhinisha Septemba 27 ,Ijumaa hii kuwa siku ya mapumziko kusherehekea ushindi wa kipusa huyoi mwenye umri wa miaka 23.

Share This Article