Bilionea wa India Adani ashtakiwa New York kwa sakata ya kutapeli mabilioni

Dismas Otuke
2 Min Read

Bilionea wa India Gautam Adani na washirika wake wengine wakuu wameshtakiwa mjini New York, Mrekani kwa kuhusika katika sakata ya utapeli wa mabilioni ya dola kwa mujibu wa kitengo cha sheria nchini Marekani.

Vyombo vya dola nchini Marekani vimeripoti kuwa Adani na wadau wake wa kibiashara saba akiwemo mpwawe Sagar Adani, waliahidi kutoa hongo ya zaidi ya dola bilioni 250 za Kimarekani ili kupewa kandarasi za kununua Solar panels.

Yamkini hongo hiyo ililengwa kuhadaa benki na wawekezaji kuchangisha hela hizo ili kuepuka sheria. Hii ni kulingana na taarifa ya Naibu Mwanasheria Mkuu Lisa Miller iliyotolewa jana.

Adani anaorodheshwa kuwa tajiri wa pili mkubwa zaidi barani Asia akiwa na zaidi ya dola bilioni 85 akimiliki kampuni ya Adani Group.

Zabuni hiyo ya kusambaza paneli za umeme jua ilikisiwa kuleta faida ya zaidi ya dola bilioni 2 kwa kipindi cha miaka 20.

Adani anadaiwa kukutana na afisa mmoja wa serikali nchini India ili kupanga njama hiyo iliyotokea kati ya mwaka 2020 na 2024.

Adani amesaini mkataba wa uwekezaji katika kampuni ya kusambaza umeme ya humu nchini, KETRACO  kwa kipindi cha miaka 30 wa kima cha shilingi bilioni 96, ambao utekelezwaji wake umepigwa breki na mahakama kufuatia kesi iliyowasilishwa kupinga mpango huo.

Share This Article