Biden na Macron wafanya majadiliano

Marion Bosire
2 Min Read

Kiongozi wa nchi ya Ufaransa Emmanuel Macron alimlaki mwenzake wa Marekani Joe Biden Jumamosi Juni 7, 2024 jijini Paris.

Biden ambaye yuko kwenye ziara nchini Ufaransa na mwenyeji wake walijadiliana kuhusu yanayoendelea mashariki ya kati na Ukraine na biashara.

Waliamua kwamba nchi hizo mbili zitashirikiana katika juhudi za kuhakikisha vita vya Israel na kundi la Hamas havisambai katika eneo zima la mashariki ya kati.

“Tunaongeza juhudi za pamoja ili kuzuia vita vya eneo zima hasa katika eneo la Lebanon.” alisema Macron huku wote wawili wakikubaliana na mpango wa uokozi wa wanajeshi wa Israel wa mateka wanne waliokuwa wameshikiliwa na Hamas tangu Oktoba 2023.

Biden alisema kwamba hawatakomesha juhudi zao hadi mateka wote waachiliwe huru na vita vikomeshwe kabisa.

Biden amekuwa akiunga mkono Israel ambayo inapigana na Hamas baada ya kundi hilo kuvamia Israel Oktoba 7, 2023 lakini vifo vya wapalestina wengi vimevuruga uungwaji mkono wa Biden kati ya wanasiasa wa mrengo wa kushoto nchini Israel jambo ambalo sio zuri wakati anapambana na Donald Trump kwenye uchaguzi mwezi Novemba.

Biden na Macron, ambao wamekuwa pamoja kwenye maadhimisho ya 80 ya D- Day siku ambayo wanajeshi walivamia fuo za Normandy ili kusaidia Uingereza kushinda Nazi, hawakukubali maswali kutoka kwa wanahabari hiyo jana.

Hafla ya maadhimisho ilianza na sherehe kwenye eneo la Arc de Triomphe,jijini Paris ambapo viongozi walitoa heshima zao kwenye kaburi la mwanajeshi mmoja wa wakati huo alizikwa.

Baadaye Biden, Macron na wake zao walielekea Elysee. Walimaliza siku kwa dhifa katika makazi ya Rais jijini Paris ambapo watu wengi mashuhuri walikuwa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *