Biden atumai vita vitasitishwa Gaza kabla ya mwezi wa Ramadhan

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Marekani Joe Biden .

Rais Joe Biden wa Amerika amesema anatumai kuwa makubaliano ya kusitisha vita huko Gaza, yatafikiwa kabla ya kuanza kwa mwezi mtukufu Ramadhan.

Maadhimisho ya mwezi huo ambapo waisilamu hufunga kula kuanzia alfajiri hadi jioni,yataanza tarehe 10 au 11 mwezi huu.

Hayo yanajiri huku majadiliano ya kina yakiendelea kuhusu kusitishwa kwa mapigano hayo naye Biden akishinikizwa kusaidia katika juhudi za kusitisha vita hivyo huko Gaza.

Duru ziliambia shirika la habari la Reuters kuwa kuna pendekezo la kusitisha makabiliano hayo kwa muda wa siku 40 wakati wa kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadan na kuruhusu kupelekwa kwa misaada ya kibinadamu huko Gaza.

Mapendekezo hayo pia yanajumuisha kuachiliwa kwa wafungwa kumi wa kipalestina kwa kila mateka mmoja wa Isreal atakayewachiliwa.

TAGGED:
Share This Article