Bibi Peng Liyuan ahudhuria shughuli ya utamaduni na michezo kwa vijana wa China na Marekani

Martin Mwanje
1 Min Read
Bibi Peng Liyuan ahudhuria shughuli ya utamaduni na michezo kwa vijana wa China na Marekani
Mke wa Rais wa China Bibi Peng Liyuan tarehe 24 Septemba alihudhuria shughuli ya utamaduni na michezo kwa vijana wa China na Marekani, yenye kauli mbiu ya “Urafiki na Ushirikiano wa Vijana kati ya China na Marekani” iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Nambari Nane ya Beijing.

Bibi Peng Liyuan alifanya mazungumzo na ujumbe wa vijana kutoka Jimbo la Washington la Marekani, akiwakaribisha China na kuifahamu China halisi. Amewataka vijana wa China na Marekani waelewane na kuwasiliana, na kuingiza nguvu chanya kwenye uhusiano kati ya China na Marekani.

Bibi Peng Liyuan ameongeza kuwa vijana watatoa mchango mkubwa kwa mustakabali wa uhusiano kati ya China na Marekani, anawataka vijana hao wa Marekani waelezee wenzao hadithi za matembezi nchini China, kuwawasilisha salamu za kirafiki kutoka watu wa China, na kuzidisha urafiki kati ya watu wa China na Marekani.

Share This Article