Benki ya Maendeleo barani Afrika, AfDB imeidhinisha mkopo wa dola milioni 110.5 kwa Kenya.
Fedha hizo zitatumiwa kusambaza umeme, kuboresha miundombinu ya kijamii na kuimarisha biashara ndogo.
Kulingana na AfDB, mkopo huo umetengewa awamu ya tatu ya mradi wa usambazaji umeme wa Last Mile Connectivity.
Benki hiyo imesema jumla ya biashara ndogo na za kati 10,521, zitapigwa jeki ikiwemo vituo vya elimu 23, vituo vya afya 15 na vituo vinane vya kusambaza maji.