Belouizdad na Ahly waumiza nyasi bila madhumuni

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa watetezi wa taji ya Ligi ya Mabingwa Afrika klabu ya Al Ahly na CR Belouizdad ya Algeria, waliambulia sare tasa katika mchuano wa raundi ya nne wa kundi D uliosakatwa Ijumaa usiku mjini Algiers.

Matokeo hayo yaliacha kundi hilo wazi zikisalia mechi mbili kukamilika kwa hatua ya makundi.

Ahly wangali kileleni pa kundi D kwa alama 6 wakifuatwa na Belouizdad na Young Africans ya Tanzania kwa alama 5 kila moja, wakati Medeama ya Ghana ikiwa ana alama 4.

Medeama watawaalika Ahly Februari 24 huku Young Africans wakiwa nyumbani Dar dhidi ya Belouizdad katika raundi ya tano.

Website |  + posts
Share This Article