Beijing kuandaa mashindano ya Riadha Duniani mwaka 2027

Dismas Otuke
1 Min Read
World Athletics Indoor championships, Glasgow 24 Council meeting at Voco hotel glasgow

Mji wa Beijing China umeteuliwa kuandaa mashindano ya Riadha Duniani mwaka 2027.

Beijing itakuwa mwenyeji wa makala hayo ya 21, miaka 12 tangu mashindano hayo yalipoandaliwa katika jiji hilo.

Uamuzi huo umeafikiwa  siku ya Alhamisi Februari 28, wakati wa kikao cha 234 cha baraza kuu la shirikisho la Riadha Duniani mjini Glasgow, Scotland.

Kikao hicho kiliandaliwa kabla ya kuanza kwa mashindano ya Riadha ya Dunia ya ukumbini, yatakayofanyika mjini Glascow kati ya tarehe 1 na 3 mwezi Machi.

China pia  itaandaa mashindano ya Riadha ya Dunia ya ukumbini mwaka 2025 katika mji wa Nanjing.

Mwaka jana, makala ya mashindano ya Riadha Duniani yaliandaliwa mjini Budapest, Hungary huku Tokyo, Japani ikitarajiwa kuandaa mashindano ya mwaka 2025.

Share This Article