Bei za mafuta zapungua kwa mwezi wa pili mfululizo

Tom Mathinji
1 Min Read

Halmashauri ya kudhibiti Bidhaa za Petroli nchini, EPRA imetangaza kupunguzwa kwa bei za mafuta katika tathmini yake ya hivi punde.

Kulingana  na EPRA, bei ya mafuta ya petroli na dizeli imepungua kwa shilingi tano mtawalia, huku bei ya mafuta taa ikipungua kwa shilingi 4.82.

Jijini Nairobi, lita moja ya petroli sasa itauzwa kwa shilingi 207.36, dizeli shilingi 196.47 na mafuta taa shilingi 194.23.

“Katika kipindi cha tathmini, bei ya lita moja ya petroli na dizeli imepungua kwa shilingi tano, huku bei ya lita moja ya mafuta taa ikipungua kwa shilingi 4.82,” ilisema EPRA kupitia taarifa.

Jijini Mombasa, lita moja ya mafuta ya  petroli itauzwa kwa shilingi 204.30, dizeli shilingi 193.41 nayo lita moja ya mafuta taa itauzwa kwa shilingi 191.05.

Kupungua kwa bei ya mafuta kwa mwezi wa pili mfululizo, huenda kumetokana na kupungua kwa mafuta ambayo hayajasafishwa katika soko la kimataifa.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article