Bei ya petroli yapungua kwa shilingi nane

Tom Mathinji
1 Min Read
Bei za mafuta zapungua.

Bei ya lita moja ya mafuta ya petroli imepungua kwa shilingi 8.18, kulingana na bei mpya zilizotangazwa na halmashauri ya nishati na kudhibiti bidhaa za mafuta (EPRA).

Katika bei hizo mpya zilizotangazwa leo Jumatatu, bei ya lita moja ya diesel na mafuta taa pia zimepungua kwa shilingi  3.54 na shilingi 6.93 mtawalia,  kuanzia Oktoba 15 hadi Novemba 14, 2024.

Lita moja ya mafuta ya petroli Jijini Nairobi itauzwa shilingi 180.66, diesel shilingi 168.06 na mafuta taa shilingi  151.39.

Jijini Mombasa, lita moja ya petroli itauzwa shilingi 177.42, diesel shilingi 164.82 na mafuta taa shilingi 148.15.

Upungufu huo umetajwa kutokana na kupungua kwa gharama ya mafuta yaliyoagizwa kati ya mwezi Agosti na Septemba.

TAGGED:
Share This Article