Bei ya ngano yaongezeka ulimwenguni kufuatia tangazo la Urusi

Marion Bosire
1 Min Read

Bei ya ngano imeongezeka sana katika masoko ulimwenguni kufuatia tangazo la Urusi kwamba italenga meli zitakazokuwa zikielekea kwenye bandari za Ukraine.

Urusi ilijiondoa wiki hii kwenye mkataba wa kuruhusu usafirishaji wa nafaka kupitia Bahari Nyeusi.

Msemaji mmoja wa Ikulu ya Marekani aliilaumu Urusi kwa kupanga kuiwekea lawama Ukraine kwa mashambulizi dhidi ya meli za raia.

Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema atarejelea mkataba wa usafirishaji nafaka iwapo matakwa yake yatatekelezwa. Matakwa hayo ni pamoja na kurejeshwa kwa benki ya kilimo ya nchi hiyo kwenye mfumo wa malipo wa ulimwengu.

Shambulizi la ndege kwenye mji wa bandari wa Ukraine wa Mykolaiv lilisababisha kujeruhiwa kwa watu 18 jana Jumatano usiku kulingana na afisa mmoja wa serikali.

Gavana wa eneo hilo Vitaliy Kim alielezea kwamba watu 9 kati ya waliojeruhiwa, wakiwemo watoto watano, walipelekwa hospitalini kwa matibabu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *