Bei ya mafuta taa, petroli na dizeli yapungua kwa shilingi moja kwa lita

Martin Mwanje
2 Min Read

Ni afueni kwa Wakenya japo kiduchu baada ya bei za mafuta taa, petroli na dizeli kupungua kwa shilingi moja kwa lita. 

Bei mpya zilizotangazwa leo Jumatano na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Bidhaa za Mafuta Nchini, EPRA Daniel Kiptoo zitatumika kati ya Februari 15 – Machi 15, 2024.

Kiptoo amehusisha kupungua huko na kupungua kwa bei za kuagiza mafuta hayo nchini.

Kutokana na hatua hiyo, mafuta ya petroli jijini Nairobi sasa yatauzwa kwa shilingi 206.36 kwa lita, dizeli kwa shilingi 195.47 kwa lita huku mafuta taa yakiuzwa kwa shilingi 193.23 kwa lita.

Wakazi wa Mombasa watanunua mafuta ya petroli kwa shilingi 203.3 kwa lita, dizeli kwa shilingi 192.41 kwa lita huku mafuta taa yakiuzwa kwa shilingi 190.05 kwa lita.

Jijini Nakuru, wakazi watanunua mafuta ya peroli kwa shilingi 205.35 kwa lita, dizeli kwa shilingi 194.88 kwa lita huku mafuta taa yakiuzwa kwa shilingi 192.66 kwa lita.

Mjini Eldoret, mafuta ya petroli yatauzwa kwa shilingi 206.12 kwa lita, dizeli shilingi 195.65 kwa lita huku mafuta taa yakiuzwa kwa shilingi 193.43.

Jijini Kisumu, wakazi watalazimika kugharimika shilingi 206.12 kwa kila lita moja ya mafuta ya petroli, shilingi 195.64 kwa kila lita ya dizeli huku mafuta taa yakigharimu shilingi 193.42 kwa lita.

Mjini Mandera, wakazi watagharimika shilingi 220.36 kwa kila lita ya petroli, shilingi 209.47 kwa kila lita ya dizeli na shilingi 207.23 kwa kila lita ya mafuta taa.

 

TAGGED:
Share This Article